Home Azam FC BAADA YA KUUMALIZA MSIMU ULIOPITA AKIWA HOI …PRINCE DUDE KAJITIKISA NA KUFUNGUKA...

BAADA YA KUUMALIZA MSIMU ULIOPITA AKIWA HOI …PRINCE DUDE KAJITIKISA NA KUFUNGUKA HAYA KUHUSU AZAM FC…


Supastaa wa Azam FC, raia wa Zimbabwe, Prince Dube amesema msimu ujao amepanga kurejesha upya makali yake katika Ligi Kuu Bara itakaponza mwezi ujao.

Msimu uliokwisha haukuwa mzuri kwa Dube ambaye hakuwa na mwendelezo wa ubora wa kiwango kutokana na majeraha ya mara kwa mara yaliyoanza kumuandama miezi michache tangu alipojiunga na matajiri hao wa Chamazi misimu miwili iliyopita.

Katika msimu wa kwanza mchezaji huyo aling’ara kwenye kikosi hicho baada ya kupachika mabao 14 na kuwa mpachikaji mabao namba tatu nyuma ya washambuliaji wa Simba, John Bocco aliyefunga 16 na Chris Mugalu 15.

Upepo haukuwa mzuri kwa Dube msimu uliokwisha ambapo alipachika mabao mawili pekee, jambo ambalo lilisababisha mchezaji huyo kufunguka kwamba anahitaji kurudisha ubora wake msimu ujao.

“Msimu uliopita ulikuwa mgumu kwangu na hata kwenye timu yetu. Hatukufikia malengo mengi japo tunafarijika kumaliza ligi kwenye nafasi tatu za juu.

“Kwangu kikwazo kikubwa ilikuwa ni majeraha ya mara kwa mara lakini sasa niko fiti. Naendelea na mazoezi kwa morali ya juu ili msimu ujao niwe bora zaidi,” alisema Dube anayeichezea pia timu ya taifa ya Zimbabwe.

Mchezaji huyo ni miongoni mwa mastraika wanne wa Azam sambamba na Shaaban Chilunda, Idris Mbombo na Rogers Kola wanaompa matumaini ya kufanya vizuri kocha mkuu wa timu hiyo, Abdhimid Moallin kutokana na ubora wa kila mmoja.

“Nina wachezaji bora zaidi ya watatu kwenye eneo la ushambuliaji, ndio maana kwenye usajili wa msimu huu hatujasaini straika kwani waliopo wanatosha,” alisema Moallin akiwazungumzia mastraika hao. Azam ipo nchini Misri kwenye mji wa El Gouna ikiendelea kujifua kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya itakaposhiriki mashindano ya ndani na Kombe la Shirikisho Afrika. 

SOMA NA HII  ARSENAL vs EVERTON..MECHI YA KUAMUA HATMA YA TOP 4 KWA ARTETA...BIRIANI LOTE HILI NI NDANI YA DStv KWA 9900 TU...