Home news MKUTANO MKUU SIMBA:..OFISI ZA SIMBA KARIAKOO KUBADILISHWA..KWA MWAKA ZITAINGIZA TSH 500 MLN...

MKUTANO MKUU SIMBA:..OFISI ZA SIMBA KARIAKOO KUBADILISHWA..KWA MWAKA ZITAINGIZA TSH 500 MLN ..


Wanachama wa klabu ya Simba wametumia saa 2 kwenye mkutano mkuu uliofungwa dakika chache zilizopita jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, ulioanza saa 4:02 asubuhi na kufikia tamati saa 6:00 mchana, wanachama wa klabu hiyo walijadili ajenda 10 kati ya 11 ambazo zilianishwa awali.

Ajenda ambayo haikujadiliwa ni 10 ya kupokea na kujadili mapendekezo ya marekebisho ya kanuni za uchaguzi na katiba ya klabu.

Katika ajenda hiyo, meza kuu ilibainisha kwamba haikupata mapendekezo ndani ya siku 21 kama ilivyotakiwa.

Kati ya ajenda 10 zilizojadiliwa kwenye mkutano huo uliofunguliwa na Mussa Azan Zungu aliyekuwa mgeni rasmi, ni hotuba ya mwenyekiti, kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kutoka bodi ya wakurugenzi na kupokea taarifa ya fedha zilizokaguliwa za mwaka uliopita 2020.


Katika mkutano huo Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amebainisha kwamba klabu ina mpango wa kujenga ukumbi wa mikutano na ofisi kwenye jengo lao lililopo Kariakoo, Msimbazi.

“Awali jengo hili ambalo ni moja ya vitega uchumi vya klabu lilikuwa likiingiza Sh200 milioni kwa mwaka, lakini sasa linaingiza Sh500 Milioni na tumezungumza mwekezaji ili klabu ijenge ofisi na ukumbi kwenye jengo hilo.

“Mchakato utaanza Januari na ujenzi utakapokamilika wapenzi na wanachama wa Simba watapata fursa ya kutembelea makao makuu ya klabu na kujionea mambo mbalimbali,” amesema.

SOMA NA HII  TUKIO LA MANULA KUTOKWA DAMU MKONONI GHAFLA KABLA YA MECHI YA JANA...ISHU NZIMA KUMBE IKO HIVI...SHABIKI ATAJAWA..