Home news MANULA, KAPOMBE, BOCCO USO KWA USO NA KOCHA MPYA SIMBA LEO…BANDA NA...

MANULA, KAPOMBE, BOCCO USO KWA USO NA KOCHA MPYA SIMBA LEO…BANDA NA DUNCAN BADO SANA…


WAKATI wachezaji tisa waliokuwa katika majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakijumuika na wenzao kuingia kambini leo jioni nyota watano watakosekana.

Kikosi hicho kinaingia kambini kwa mara ya kwanza toka kocha wao mpya Pablo Franco ajiunge na kikosi hicho akichukua nafasi ya Didier Gomes aliyeachana na Simba baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nyota wa Simba waliokuwa katika majukumu ya Kitaifa ni Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala, Israel Mwenda, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin, Kibu Denis pamoja na John Bocco.

Wengine ni Meddie Kagere, Peter Banda, Duncan Nyoni pamoja na Larry Bwalya huku Thadeo Lwanga pamoja na Chris Mugalu wakiwa majeruhi kwa sasa.

Baada ya mazoezi ya leo jioni katika uwanja wa Boko kikosi kitaingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Novemba 19 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Kikosi cha Simba kiliendelea na maandalizi kwa wachezaji ambao walisalia baada ya wenzao kuwepo katika timu zao za Taifa.

Nyota watatu katika kikosi hicho Bwalya, Duncan pamoja na Banda hawataingia kambini kutokana na majukumu yao katika timu zao za Taifa ambazo zinakamilisha ratiba kesho.

Banda na Duncan watakuwa na timu yao ya Malawi ambayo itakuwa ugenini dhidi ya Msumbiji huku Bwalya atakuwa pia ugenini na timu yake ya Zambia ambao wataumana na Tunisia.

SOMA NA HII  WAKATI KUKIWA NA MJADALA WA KUFUNGA VAR...AHMED ALLY AMJIBU WAZIRI WA FEDHA MH MWIGULU 'KIBABE'