Home CAF KUELEKEA MECHI YA CAF….KIKOSI CHA WASAUZI CHAANZA KUPUKUTIKA…BEKI WAO WA ‘KAZI CHAFU’...

KUELEKEA MECHI YA CAF….KIKOSI CHA WASAUZI CHAANZA KUPUKUTIKA…BEKI WAO WA ‘KAZI CHAFU’ AUMIA…


Beki wa kushoto wa Orlando Pirates Paseka Mako aliondolewa uwanjani hapo jana kwa gari la wagonjwa baada ya kuumia katika mechi ya DStv Premiership dhidi ya Baroka FC kwenye Uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane.

Mako alikuwa amepoteza fahamu na alipatiwa huduma ya kwanza na wahudumu wa kabla ya kuondolewa uwanjani kwa gari la wagonjwa na kupelekwa hospitalini.

Taarifa kutoka Pirates zinasema β€œKufuatia jeraha la dharura lililomhusisha beki Paseka Mako kwenye mechi ya DStv Premiership dhidi ya Baroka FC jana usiku, Klabu ya Orlando Pirates inaweza kuthibitisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 yuko katika hali nzuri.

“Daktari amefichua kuwa matokeo ya uchunguzi wa CAT hayajaonyesha dalili za kuvunjika kwa fuvu la kichwa au kuvuja damu kwenye ubongo. Hata hivyo, mchezaji huyo amepata jeraha kwenye uso na pua.

Orlando wanatarajia kucheza mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba Aprili 17 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  WAKATI WATU WAKIHISI PENGINE NI MORRISON..SENZO AFUNGUKA SABABU KUBWA YA KUTEMANA NA YANGA...ADAI HAKUWA NA JINSI ZAIDI YA KUFANYA HIVYO...