Home Uncategorized COASTAL UNION YAMKOMALIA KIBA

COASTAL UNION YAMKOMALIA KIBA


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa nyota wa timu hiyo ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva Ally Kiba yupo sana ndani ya kikosi hicho.

Kiba msimu uliopita ndani ya Coastal Union alicheza mechi mbili tu kutokana na kubanwa na majukumu ya kazi za muziki.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye harakati ya kusuka kikosi upya hawana mpango wa kumuacha Kiba.

“Kiba ni mchezaji mzuri uwezo wake upo wazi licha ya msimu uliopita kubanwa na majukumu hatuna mpango wa kumuacha tupo naye kwenye mazungumzo ili tujue namna ya kupanga ratiba zake,” amesema Mgunda.

SOMA NA HII  KOCHA MANCHESTER UNITED: TULISTAHILI USHINDI