Home Uncategorized NAFASI YA HAJI MANARA SIMBA YAGOMBEWA KWA KASI YA KUTISHA

NAFASI YA HAJI MANARA SIMBA YAGOMBEWA KWA KASI YA KUTISHA


BAADA ya Simba kutangaza nafasi za kazi hivi karibuni kwa vitengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kitengo cha Media Officer (Ofisa Habari), Chief Executive Officer (Mtendaji Mkuu), Technical Director (Mkurugenzi Ufundi) imeelezwa kuwa ya kitengo cha Habari inagombewa kwa kasi.


Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa wengi sana wanaulizia habari ya kitengo cha Habari kilicho chini ya Haji Manara.

“Watu wanaendelea kutuma maombi ya kazi ila wengi wamejitokeza kuomba kazi kwenye kitengo cha Media Officer, nadhani wataendelea kufanya hivyo mpaka muda wa maombi utakapofungwa,” amesema.
SOMA NA HII  SIMBA YAIPOTEZA MAZIMA YANGA NDANI YA DAKIKA 270