Home Uncategorized AZAM FC KUKWEA PIPA KESHO KUELEKEA RWANDA

AZAM FC KUKWEA PIPA KESHO KUELEKEA RWANDA


KOCHA Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije ameahidi kutetea ubingwa wa kombe la Kagame ambalo linatarajiwa kuanza Julai 7-21 nchini Rwanda.

Azam FC ni watetezi wa kombe wamepangwa kundi B pamoja na KCCA (Uganda), Mukura (Rwanda) na Bandari (Kenya) wanatarajiwa kukwea pipa kesho kutia timu nchini Rwanda.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wanakwenda wakiwa kifua mbele kupambana kutetea ubingwa kwa mujibu wa kocha Ndayiragije ambaye tayari ameanza kukinoa kikosi hicho. 

SOMA NA HII  KOCHA MANCHESTER UNITED YADAIWA CHANZO LUKAKU KUSEPA