Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA MAZEMBE…MANARA ‘AWAPA ZA USO’ MASHABIKI YANGA KWA KUONYESHA UONYONGE..

KUELEKEA MECHI NA MAZEMBE…MANARA ‘AWAPA ZA USO’ MASHABIKI YANGA KWA KUONYESHA UONYONGE..

Habari za Yanga

Haji Manara amewashangaa mashabiki na wanachama wa Yanga SC kuonekana wanyonge kipindi hiki ambacho timu hiyo inajiandaa na mchezo wake dhidi ya TP Mazembe Benjamin Mkapa Jumapili ya Februari 19, 2023.

”Kwa nini tunakuwa Wanyonge Wananchi?. Kwa nini tunashindwa kuwaambia Watu juu ya ubora wa Wachezaji wetu?”

”Tutumie ubora wa Wachezaji wetu tulionao kuwajenga Washabiki wetu kwamba Mazembe hatoboi na hii itasaidia kuwavuta zaidi uwanjani. Silaha kubwa katika mechi kama hizi ni confidence ya Washabiki na Wachezaji wenyewe ,tusikubali unyonge hata kidogo.”

”Tuwape promo Wachezaji na tuwape nguvu ya kujiamini, hawa Wachezaji wanasoma sana mitandao na wanapenda sana kuandikwa Kwa mema yao kama tulivyo Binadamu wote, tujikite huko na tusikubali kushindwa na Wapinzani wetu ndani ya Uwanja kwa idadi ya Wafuasi weekend hii.”

”Hamasa iwe juu Kwa kila mmoja wetu, dunia ya social media tuitumie ipasavyo, na tusiwaangalie nn wenzetu wanafanya, tujikite kutengeneza maudhui itakayovuta Wananchi jumapili, moja wapo ni kutumia hata celebrities wetu kutusaidia katika kuvuta washabiki Jumapili.

“Na katika hili pamoja na kufungiwa kwangu nitalifanya kwa maslahi maalum ya jumapili,,nitakutana nao haraka ili tuone wanasaidiaje kupush hii hamasa,,,najua nchi itaelewa dhamira yetu njema. Kila Mwanayanga now amhamasishe mwenzie kuja Kwa Mkapa siku hiyo.”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI