Home Habari za michezo BAADA YA KUVURUNDA MECHI NA HOROYA…SIMBA WAMTUMA BOCCO KUFUNGUKA HAYA…

BAADA YA KUVURUNDA MECHI NA HOROYA…SIMBA WAMTUMA BOCCO KUFUNGUKA HAYA…

Habari za Simba

Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco amesema, wameutumia mchezo wao wa Kimataifa uliopita dhidi ya Horoya ya Guinea kama somo kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Raja Casablanca.

Nahodha huyo ameyasema hayo mapema leo Februari 17, 2023 kwenye mkutano wa wanahabari kuelekea mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni mechi ya pili katika hatua ya makundi.

Bocco amesema, kwenye mchezo huo kuna mazuri waliyafanya na kuna mapungufu hivyo wameshayafanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi na wanaamini kesho wanakwenda kuibuka na pointi tatu katika uwanja wa nyumbani, Benjamini Mkapa Studium.

“Kuna mazuri tuliyoyafanya kwenye mchezo ule tunakwenda kuyaboresha zaidi na yale mapungufu pia tumeshayafanyia kazi. Mpira ni mchezo ambao ukifanya makosa unaadhibiwa hivyo tumejiandaa vizuri na kuongeza umakini kwenye eneno la ulinzi na hata kushambulia pia,” alisema Bocco.

Mchezo wa awali dhidi ya Horoya, Simba SC alipoteza kwa bao 1-0 ugenini na sasa anarejea nyumbani kutupa karata yake ya pili.

SOMA NA HII  ALLY KAMWE:- OKRAH ANA STRESS SANA...