Home Habari za michezo ALLY KAMWE:- OKRAH ANA STRESS SANA…

ALLY KAMWE:- OKRAH ANA STRESS SANA…

Habari za Yanga leo

Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema, mchango anaoutoa kiungo wao mshambuliaji Augustine Okrah bado hajachanganya sababu bado ana stress lakini ipo siku atakuwa balaa zaidi.

Kamwe ametoa kauli hiyo juzi Februari 20, 2024 baada ya nyota huyo raia wa Ghana kukiwasha kwenye mchezo wa Azam Sports Federation dhidi ya Polisi Tanzania na Okrah kutoa asist mbili katika ushindi wa 5-0 walioupata.

“Okrah bado ana stress alizowahi kuzipata hapa nchini, hata hizi asist mbili alizopata leo, bado hajacheza kwenye kiwango kile anachoweza kucheza akiwa hana stress, ametuhakikishia ipo siku inakuja ambayo stress itakwisha na atafanya balaa,” alisema Kamwe.

Kesho Yanga itashuka tena dimbani kukipiga na CR Beoulzidad katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku wakihitaji ushindi kwa hali na mali.

Kuelekea mchezo huo, Yanga wamejizatiti vyema huku wakiupa jina la Pacome day pamoja na kufanya hamasa mbalimbali kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

SOMA NA HII  KISA MECHI YA SIMBA vs YANGA....VAR KUANZA KUTUMIKA KWENYE MECHI ZA LIGI KUU BONGO...