Home Habari za michezo HIVI NDIVYO MORRISON ANAVYOITAFUNA YANGA MAMILIONI KIULAIINI KABISA…WALA HAJALI YANI…

HIVI NDIVYO MORRISON ANAVYOITAFUNA YANGA MAMILIONI KIULAIINI KABISA…WALA HAJALI YANI…

Habari za Yanga

Yanga inashuka dimbani kesho kutwa jumapili kupambana na TP Mazembe ukiwa ni mchezo wa pili baada ya wa kwanza kufungwa goli 2-0  huku mchezaji wake Mghana Benard Morrison akiwa hajaambatana na timu kutokana na aliyonayo.

Kwa Mujibu wa Ofisa habari wa Yanga Ali Kamwe, Morrison ana majeraha yatakayomweka nje kwa miezi miwili.

Pamoja na majeraha hayo, Morrison amekuwa kama vile anaipiga Yanga pesa kwani muda mwingi tangu amerejea kwa Wanajangwani hao mwanzoni mwa msimu huu amekuwa nje ya uwanja kwa sababu mbalimbali kuliko kuitumikia timu.

Inafahamika staa huyo ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mrefu zaidi Yanga, akichukua Dola 10,000 ambazo ni sawa na Sh23,450,000 za Kitanzania lakini ni muda mchache sana aliovuja jasho uwanjani kuitumikia pesa hiyo na kutoa matokeo chanya.

Morrison hadi sasa ameichezea Yanga mechi 10 tu kwenye ligi na kati ya hizo amecheza jumla ya dakika 541 tu kwani ni mchezo mmoja pekee aliomaliza dakika zote 90, ule wa duru ya kwanza dhidi ya Azam FC.

Katika mechi hizo 10 alizocheza, amefunga mabao mawili tu, moja dhidi ya Coastal Union mechi ya pili ya ligi dakika ya nne na lingine ni lile la penalti dakika ya 45 alilofunga dhidi ya Geita Gold kwenye mzunguko wa kwanza pale Kirumba Mwanza, Yanga ikishinda kwa bao hilo hilo moja.

Mwamba huyu ametoa asisti tatu tu hadi sasa, moja ikiwa ile aliyompa Bakari Mwamnyeto akifunga bao la pili kwenye ushindi wa 2-0 mbele ya Polisi Tanzania katika mzunguko wa kwanza na nyingine alimpasia Jesus Moloko na kufunga bao la kwanza kwenye mechi dhidi ya Namungo katika ushindi wa 3-0.

Katika mechi za kimataifa (CAF), ambazo ndiyo lengo kuu la Yanga kumsajili Morrison, amecheza mbili tu hadi sasa na zote hakumaliza dakika 90.

Katika mechi mbili za hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan FC zote hakuwepo hata benchi na kuanza kucheza hatua ya mwanzo dhidi ya Al Hilal ya Sudan inayonolewa na kocha wake wa zaman Florent Ibenge.

Kwenye mechi ya kwanza iliyopigwa Kwa Mkapa na kumalizika kwa sare ya 1-1, Morrison alianza katika kikosi cha kwanza na kutolewa dakika ya 78 nafasi yake ikichukuliwa na Farid Mussa na ile ya marudiano ugenini ambayo Yanga ilicheza na kuchapwa 1-0, Morrison alianza na kutoka dakika ya 77 akimpisha Herritier Makambo.

Baada ya hapo Yanga ilidondokea Kombe la Shirikisho kupangiwa mechi za mtoano dhidi ya Club Africain ya Tunisia na mchezo wa kwanza ulipigwa kwa Mkapa na kumalizika kwa suluhu 0-0, alianza kikosini lakini dakika ya 62 alitolewa na kuingia Farid Mussa huku kwenye ule wa marudiano ambao Aziz Kii alifunga bao moja na la ushindi (1-0) na Yanga kutinga Makundi alianza lakini akatoka dakika ya 89 akiingia Bakari Mwamnyeto.

Kiufupi kwenye CAF, Morrison amecheza dakika 306 katika mechi nne kati ya sita chama lake lilizocheza hadi sasa na huenda asicheze mchezo hata mmoja kati ya sita ijayo ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi kutokana na kuwa majeruhi.

Kwa maana hiyo Morrison tangu amerejea kikosini hapo ameichezea Yanga Jumla ya dakika 849 tu kwenye Ligi na CAF, huku timu hiyo ikicheza mechi 28 ambazo ni sawa na dakika 2520 kwenye mashindano hayo mawili hivyo amekosa dakika 1673 ambazo ni karibu robo tatu ya zile alizocheza.

Hadi sasa Morrison ana mwezi wa tisa ndani ya Yanga na hadi mwisho wa mwezi huu mshahara ambao atakuwa amevuta ni Sh211,050,000 ambao ni sawa na Sh34,900 kwa kila dakika aliyocheza hivyo amewapiga Yanga zaidi ya milioni 41 (41,657,700).

SOMA NA HII  SIMBA INAKWAMA HAPA...BARBARA ALIA YAMEMKUTA..PABLO MUGALU WATOA SULUHISHO...