Home Michezo SINGIDA FOUNTAIN GATE YABADILI GIA ANGANI

SINGIDA FOUNTAIN GATE YABADILI GIA ANGANI

KLABU ya Singida Fountain Gate imefanya mabadiliko ya kambi yake ya mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa mashindano.

Awali klabu hiyo ilipanga kuweka kambi Tunisia.

“Tunapenda kuwataarifu wadau na mashabiki wa Singida Fountain Gate FC kwamba maandalizi ya msimu ujao kwa klabu yetu yatafanyikia jijini Arusha kuanzia Julai 10, 2023,”imesema taarifa ya timu hiyo.

Kwa mujibu klabu hiyo mabadiliko hayo yanatokana na ufinyu wa muda na kuchelewa kukamilika kwa usajili wa wachezaji, hivyo kulazimika kubaki nchini ili wachezaji wote waweze kushiriki maandalizi hayo kwa wakati.

SOMA NA HII  IMEFICHUKAA...HIVI NDIVYO USAJILI WA 'SURE BOY' ULIVYOIKAMUA YANGA MAMILIONI YA PESA...