Home Habari za michezo KWA TAARIFA YAKO SIMBA WAMESHAMPA THAN YOU KIYOMBO….MUDA WOWOTE ANATUA KATIKA KLABU...

KWA TAARIFA YAKO SIMBA WAMESHAMPA THAN YOU KIYOMBO….MUDA WOWOTE ANATUA KATIKA KLABU HII

Klabu ya Simba tayari imeshampa “THANK YOU” Mshambuliaji wake raia wa Tanzania Habibu Kiyombo na kilichobaki ni kumtangaza tu.

Habibu alifanya vizuri 2021-22 akiwa na Mbeya Kwanza, ameshindwa kuwaburudisha Wanasimba 2022-23.

Kwa sasa Klabu zimeshaanza kupeleka ofa Kwa Mshambuliaji huyo , huku akikataa ofa ya Mashujaa FC iliyopanda ligi msimu huu Kwa kuwashusha Mbeya City.

Inaelezwa kuwa matamanio ya nyota ni kucheza Kimataifa na kwa sasa nyavu zake amezitupa Kwa Singida Fountain Gate FC ambapo Bado mazungumzo hayajaanza.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA MTU MUHIMU SANA SIMBA....MAGORI AJITOSA KWENYE SIASA RASMI...AOMBA UBUNGE WA....