Home Habari za michezo HUO MKWARA WA SIMBA KWA ASEC SIO POA

HUO MKWARA WA SIMBA KWA ASEC SIO POA

Habari za Simba leo

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa kazi yao kubwa ni kupata ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.

Mchezo huo wa hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 25 2023.

“Tunakazi moja tu ya kumnyoa ASEC Mimosas, tunatambua wapinzani wetu wataleta ushindani lakini tutapambana kufanya vizuri.

“Kikubwa Wanasimba wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu muhimu kwa kuwa wao ni muhimu kuongeza nguvu kwa wachezaji kupambana na kupata matokeo mazuri.

“Tupo nyumbani na huu ni mchezo muhimu kwetu kuanza safari ya kuyafuata malengo yetu mashabiki tuzidi kuwa pamoja a kushirikiana kama ambavyo sera yetu ya nguvu moja inasema,”.

SOMA NA HII  EYMAEL AKUTANA NA RUNGU LA TFF, YAMKAMUA MILIONI 8