Home Uncategorized EYMAEL AKUTANA NA RUNGU LA TFF, YAMKAMUA MILIONI 8

EYMAEL AKUTANA NA RUNGU LA TFF, YAMKAMUA MILIONI 8

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungua miaka miwili aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael kujihusisha na masuala ya soka Tanzania.

Mbali na kufungiwa miaka miwili pia anatakiwa kulipa faini ya Shilingi milioni 8.

Yote haya ni kutokana na makosa yake ya ubaguzi pamoja na uchochezi ambayo aliyafanya baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli uliochezwa Julai 26 Uwanja wa Samora Iringa.

Eymael kwa kosa hilo alifutwa rasmi kazi na Yanga, Julai 27 na kwa sasa yupo zake Ubelgiji.

SOMA NA HII  JINSI PACOME ALIVYOINUSURU YANGA KWENYE HATARI YA WARABU