Home Uncategorized HUYU NDIYE MWILI JUMBA ALIYESHUSHWA NA YANGA KUCHUKUA NAFASI YA MAKAMBO

HUYU NDIYE MWILI JUMBA ALIYESHUSHWA NA YANGA KUCHUKUA NAFASI YA MAKAMBO

USIKU wa kuamkia leo klabu ya Yanga imeshusha mashine mpya kwa ajili ya kukamilisha usajili wake wa mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa leo.

Mchezaji huyo ambaye ni mwili jumba inaelezwa kuwa amekuja kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Heritier Makambo ambaye amejiunga na Horoya AC.

Mwinyi Zahera alisema kuwa nafasi iliyobaki ndani ya kikosi hicho ni ya mshambuliaji.

Jina lake anaitwa David Muringe ametokea klabu ya FC Lupopo pia amewahi kucheza soka la kulipwa nchini Angola msimu uliopita alitupia mabao 14 katika mechi 16 alizocheza.

SOMA NA HII  KINACHOENDELEA BAINA YA YANGA NA FALCAO - VIDEO