Home Uncategorized GWIJI MANCHESTER UNITED AMPA TANO FERNANDES

GWIJI MANCHESTER UNITED AMPA TANO FERNANDES

GWIJI wa Manchester United, Paul Scholes, amesifu mchango ulioletwa na Bruno Fernandes klabuni hapo, akisema raia huyo wa Ureno amekuja na kitu kilichokosekana kwa muda mrefu United.
Mara baada ya kujiunga akitokea Sportling Januari, Fernandes ameisaidia United kucheza mechi 11 mfululizo bila kupoteza kabla ya ligi kusimamishwa kutokana na Virusi vya Corona.
Katika mechi tisa za michuano yote akiwa na United, nyota huyo mwenye miaka 25, amefunga mabao matatu na asisti nne akikisaidia kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kuwa na muunganiko mzuri kutokea nyuma kwenda kwenye ushambuliaji.
Scholes amesema Mreno huyo ameongeza kitu kwenye safu ya kiungo ya United, ingawa anakiri kwamba bado hana uhakika ni mfumo gani unamfanya acheze vizuri zaidi.
“Haonekani kama ni kiungo wa kati kwangu mimi, namuona kama namba 10 wa kutoka na kuingia, daima anageuka na ni kiunganishi ambacho United ilikihitaji sana,” alisema Scholes.
“Walikosa ubora huo kwenye kiungo na tangu alipokuja, ameuleta. Anaweza kuwalisha mipira wachezaji, anaweza kupiga mashuti na anaonekana ni kiongozi wa kweli pia. United ilikosa mtu wa namna hiyo.
“Yupo kama Eric Cantona au Teddy Sheringham – anaweza kuwapita wapinzani pia.”
SOMA NA HII  YANGA WATAJA SABABU ZITAKAZOMPA NAFASI KAZE KUIBUKIA JANGWANI