Home Uncategorized NYOTA WA GOFU APIGA HESABU ZA KUIBUKIA KWENYE BIASHARA KUINUA KIPATO

NYOTA WA GOFU APIGA HESABU ZA KUIBUKIA KWENYE BIASHARA KUINUA KIPATO


NYOTA wa gofu Afrika Mashariki na Kati anayekipiga katika klabu ya gofu ya Lugalo jijini Dar es Salaam, Angel Eaton, amesema mipango yake hivi karibuni ni kufungua mgahawa wa chakula utakaomsaidia kuongeza kipato tofauti na anachokipata akishiriki mashindano tofauti.
Eaton amesema kuwa mchezo wa gofu haumlipi kama watu wanavyodhani ndio maana anaingia kwenye ujasiriamali.
“Ukiangalia nyumbani nimejaza makombe kibao lakini sina hata kipato cha kunifanya niridhike na haya maisha, plani zangu kichwani ni kusaka mtaji ili nianze kuuza chakula kilichokuwa na viwango vya hali ya juu.
“Biashara ya chakula naamini inalipa sababu watu lazima wale kila siku tena ukizingatia kipindi hiki michezo imesimama ndio maisha kwetu yanazidi kuwa magumu sababu hela hakuna,” amesema Eaton.
SOMA NA HII  HARMONIZE MATATANI TENA, DIAMOND ATAJWA