Home Habari za michezo BAADA YA AZIZ KI NA KAMBOLE KUMALIZANA NA YANGA….CHUMA KINGINE HIKI HAPA…CARLINHOS...

BAADA YA AZIZ KI NA KAMBOLE KUMALIZANA NA YANGA….CHUMA KINGINE HIKI HAPA…CARLINHOS AHUSIKA ‘KUSET DILI….’


KOCHA Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, ameamua kutumia ukaribu wake na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Angola, Carlos Carlinhos kumfuatilia kwa ukaribu beki wa kushoto, Joyce Lomalisa Mutambala.

Mutambala raia wa DR Congo, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Bravos do Maqui ya Angola, pia amewahi kucheza GD Interclube (Angola), AS Vita (DR Congo) na Mouscron ya Ubelgiji.

Yanga imepanga kufanya usajili wa beki wa kushoto baada ya kumkosa mbadala mzuri wa kucheza eneo hilo na kulazimika kutumiwa Kibwana Shomari ambaye ni beki wa kulia.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Kamati ya Mashindano ya Yanga, kimesema kwamba, Nabi ndiye aliyependekeza usajili wa beki wa kushoto wa kigeni kuelekea michuano ya kimataifa msimu ujao.

Mtoa taarifa huyo aliendelea kusema kuwa, wachezaji Djuma Shaban na Yanick Bangala ndio wamemshawishi Nabi kumsajili haraka Mutambala mwenye uwezo mkubwa wa kulinda goli na kuanzisha mashambulizi.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, mara baada ya kocha huyo kushawishiwa na mabeki hao raia wa DR Congo, haraka akawasiliana na Carlinhos ili kupata mafaili ya Mutambala, kabla ya kuwashawishi viongozi kumpa mkataba.

“Tunafurahia sana usajili wa msimu huu, kocha Nabi amepania kusajili wachezaji wachache na kuacha wachache, ila amesema kabla ya kuachana nao, ni vema akahakikisha anapata wachezaji bora na wenye uwezo sahihi wa kumwezesha kufikia malengo yake kimataifa.

“Kutokana na hilo, tayari amepewa mchongo na Djuma na Bangala wa kumsajili beki wa kushoto kutoka Angola, ambapo pia naye amejiridhisha ubora wake kutoka kwa aliyekuwa mchezaji wetu Carlinhos.

“Carlinhos amemtoa hofu Nabi kwa kumwambia beki huyo yupo katika ubora hivi sasa na kama akija kuichezea Yanga, basi watakuwa wamefanya usajili bora katika nafasi hiyo.

“Kutokana na hali hiyo, sasa ni wazi kuwa kama Mutambala atamaliza tatizo la upande wa kushoto, kwani kocha alikuwa anatamani sana kupata mchezaji mwenye uwezo wa kupanda na kushuka kama ilivyo kwa Djuma na Kibwana,” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  SAKATA LA MANARA GSM WATAJWA,KUNA MBUKINAFASO WA YANGA,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI