Home Habari za michezo MANARA AMLIPUA JEMEDARI SAIDI…ADAI ALIMSINGIZIA KESI YA UHUJUMU UCHUMI KIPINDI CHA RAIS...

MANARA AMLIPUA JEMEDARI SAIDI…ADAI ALIMSINGIZIA KESI YA UHUJUMU UCHUMI KIPINDI CHA RAIS MAGUFULI…


Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema kitendo chake cha kutoka Simba na kujiunga na Yanga kimekubwa na vikwazo vingi kutokana na kushambuliwa au kuandamwa sana na baadhi ya wachambuzi akiwemo mchambuzi wa soka na mwandishi wa EFM Jemedari said.

Manara amesema kipindi akiwa Simba aliwahi kupewa adhabu na TFF akiwa yeye, Hassan Bumbuli na aliyekuwa Kiongozi wa Simba Zacharia Hans Pope, katika hatua za kutekeleza malipo ya faini hiyo akapeleka pesa taslimu TFF baada ya hapo mwandishi huyo akamchongea kwa TAKUKURU kuwa anajihusisha na shughuli za utakatishaji fedha pamoja na uhujumu uchumi.

Kwa upande mwingine Manara amebainisha kuwa Yanga ilikuwa imtambulishe mchezaji mmoja siku ya jana lakini kutokana na shamrashamra za ubingwa wakaahirisha na muda wowote ule kuanzia sasa mchezaji huyo anaweza kutambulishwa.

Yanga imefanikiwa kupata ubingwa wake wa mara ya 28 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kufuatia kuwa na mwenendo mzuri sana wa Ligi tangu ilipoanza huku mshambuliaji wao Fiston Mayele raia wa Congo akiwa kinara wa mabao katika msimamo wa wafungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na mabao 16, bao moja zaidi ya mshambuliaji wa Geita Gold FC, George Mpole.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ATAJWA KUIBUKIA YANGA