Home Habari za michezo MASTAA YANGA WAFUNGUKA MAGUMU HAYA WANAYOPITIA LIGI KUU

MASTAA YANGA WAFUNGUKA MAGUMU HAYA WANAYOPITIA LIGI KUU

Geita vs Yanga

Mastaa wa Yanga wamekiri kwamba wana njia ngumu mbele yao haswa katika mechi nne mfululizo zinazofuata kwenye Ligi Kuu ya Bara.

Mechi hizo ambazo nyingi zitachezwa Dar es Salaam na moja Tanga ni ddidi ya Azam FC, Singida Big Stars yenye Kocha mpya Mbrazili, Simba Sc na Coastal Union.

Yanga ambayo ipo kambini Avic Jijini Dar es Salaam, watakuwa wenyeji wa Azam FC Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ambao timu yoyote ya ndani kuukodi kwa mechi moja ni Sh 5.9 milioni.

Wakizungumza na Mwanaspoti, mastaa wa Yanga ambo ina pointi 12 ikishikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo, wametamba kuendelea walipoishia kwa kuibuka na ushindi kwenye mechi hizo huku wakikiri kuwa ndio ngumu zitakazoamua hatma ya kutetea ubingwa wao.

Keneddy Musonda ambaye ni raia wa Zambia iliyoko kundi moja na Taifa Stars kwenye Afcon ya mwakani, alisema Azam hautakuwa mchezo rahisi kwasababu wanakutana na timu ambayo haitataka kurudia makosa, wanataka kuibuka na ushindi ili kulipa kisasi hivyo wamejiandaa vyema kuendeleza ubora wao kila wanapokutana na timu hiyo.

“Tunakutana na timu ambayo itataka kulipa kisasi na ina ubora kutokana na matokeo mazuri waliyonayo hilo halitupi shida tumejiandaa kwaajili ya kushindana lengo ni moja tu kupata matokeo yatakayotufanya tuendelee kusonga mbele kutetea taji;

“Ukiachana na Azam FC tuna ratiba nyingine ngumu kucheza na SBS na baadae Simba mechi hizo zote ni muhimu kwetu na ni za kuamua kutetea taji kwasababu ni timu ambazo mara nyingi tumekuwa tukikimbizana kwenye kutetea taji,” alisema Musonda ambaye kwa mujibu wa mitandao ya michezo ana miaka 28.

Joyce Lomalisa ambaye mbwembwe zake uwanjani kwa sasa zinawakosha mashabiki, alisema hawajiandai kwaajili ya mchezo mmoja wanajifua kulingana na ratiba yao ilivyo ngumu na ya kupambana kuhakikiha wanakuwa imara tayari kwaajili ya ushindani kwasababu wana michezo mitatu mfululizo migumu.

Alisema maandalizi yanaenda vizuri wao waka wahezaji wapo katika hali nzuri kilichobaki ni uamuzio wa dakika 90 za mchezo wamejiandaa kushinda huku akisisitiza kuwa mchezo huo ni miongoni mwa michezo itakayotoa mwanga wa ubingwa.

“Azam FC ni timu ambayo tunapambana nayo kupambania ubingwa, kuna SBS na Simba hivyo pointi tatu kutoka kwao ni muhimu zaidi ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kutetea taji tunalolishikiria,” alisema.

Kibwana Shomari ambaye ni miongoni mwa wazawa wazoefu kazini, alisema ni michezo ambayo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na namna wanavyokutana na changamoto ya ushindani kila wanapokutana.

“Tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia mchezo wetu na kutupa sapoti ya kuhakikisha tunapata matokeo mazuri yatakayotupa mwanga mzuri kwenye kutetea taji,” alisema.

“Mechi zote tunacheza Dar es Slaam isipokuwa mchezo mmoja ambao tutaenda Tanga kati ya minne ambayo ipo mbele yetu hivyo tunahitaji kuwa timamu zaidi ili kuweza kutumia vyema dakika 270 Dar es Salaam kabla ya kwenda Tanga kuwavaa Coastal Union.”

SOMA NA HII  MEDDIE KAGERE AKWAMA DAKIKA 360 BILA KUTUPIA