Home Habari za michezo HIZI HAPA SABABU YA KIFO CHA MCHEZAJI WA U17 WA SINGIDA BIG...

HIZI HAPA SABABU YA KIFO CHA MCHEZAJI WA U17 WA SINGIDA BIG STAR ALIYEFIA UWANJANI LEO..

Mchezaji Singida Big Stars afariki dunia

Kinda wa Singida Big Stars aliyefia uwanjani, Mohammed Banda anatarajiwa kuzikwa kesho saa saba mchana katika kijiji cha Mlandala wilayani Iramba mkoani Singida.

Banda alifariki mapema leo asubuhi wakati kikosi cha timu ya vijana U17 kikifanya mazoezi katika uwanja wa Magereza mkoani Singida.

Kinda huyo ambaye ni nahodha wa kikosi hicho alikuwa akigombea mpira wa juu na mshambuliaji wa timu hiyo.

Mtendaji Mkuu wa timu hiyo,Muhibu Kanu amesema kama timu wamechukua majukumu yote kuhakikisha wanamstiri mchezaji huyo na anapata heshima zote.

Amesema marehemu atazikwa kesho katika kijiji cha Mlandala wilayani Iramba mkoani Singida.

“Kesho tutatoka hapa kwenda nyumbani kwao kule Mlandala njia ya kwenda Iramba ataenda kuzikwa saa saba kamili,”amesema Muhibu.

Akisimulia jinsi ilivyokuwa Muhibu amesema kocha wa timu ya vijana aitwaye Mtipa aliamua kuweka full game ili kuangalia kile ambacho amefundisha.

“Kwenye kucheza kulikuwa na defender na striker imewekwa krosi,striker kaweka kichwa kufunga na defender kama kawaida anataka kuokoa, kwenye kuokoa wakagongana hewani,”amesema

Amesema baada ya kugongana wakaanguka chini lakini aliyeanguka vibaya zaidi ni defender ambaye ni Banda.

“Akapata huduma haraka haraka ukafanyika utaratibu wa kumpeleka hospitali na sisi tukapigiwa simu tukawahi tukamchukua tukampeleka hospitali, madaktari wamefanya kazi yao nzuri lakini wamejitahi kuokoa lakini tukampoteza,”amesema Muhibu.

SOMA NA HII  SALAH AFANYA KUFRU YA AINA YAKE KIJIJINI KWAO...AGAWA MILIONI NANE KWA KILA FAMILIA MASIKINI...