Home Habari za michezo WAKATI MASHABIKI SIMBA WAKILIA NA ‘SUB’ YA CHAMA…MBRAZILI KAWASIKIA..KISHA AKAJIBU HIVI..

WAKATI MASHABIKI SIMBA WAKILIA NA ‘SUB’ YA CHAMA…MBRAZILI KAWASIKIA..KISHA AKAJIBU HIVI..

Habari za Simba SC

Kocha Mkuu Klabu ya Simba SC,Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema ushindi wa mabao 3-2 ambao Simba iliupata hapo jana dhidi ya Mbeya City ni jambo la kwanza alilokuwa anahitaji na limemfanya afurahi.

Robertinho amesema amefurahishwa na wachezaji walivyocheza kitimu licha ya kuwa amekaa nao kwa muda mfupi.

“Ilihitajika ushindi bila kujali tumechezaje, tupo kwenye mbio za ubingwa tunapaswa kushinda kila mchezo hasa tukiwa nyumbani.

“Ndiyo kwanza nina siku nane tangu nilipoanza kazi. Simba ni timu kubwa na malengo yake ni makubwa pia kama nilivyo mimi”

“Jambo jengine lililonifurahisha ni jinsi tulivyocheza, wachezaji walicheza kitimu ingawa kulikuwa na makosa kadhaa ambayo tunapaswa kuyaondoa.

“Nimeanza kupata mwanga wa kikosi ambavyo kinapaswa kiwe,” amesema Robertinho.

SOMA NA HII  ISHU YA MORRISON KUZUIWA KUINGIA SAUZI..MASHABIKI WA SIMBA SAUZI WAIBUKA NA HILI..WATOA ONYO...