Home Uncategorized BIASHARA UNITED: TUNA HALI NGUMU ILA TUNAZITAKA POINTI ZA NDANDA

BIASHARA UNITED: TUNA HALI NGUMU ILA TUNAZITAKA POINTI ZA NDANDA


UONGOZI wa Biashara United umesema kuwa hesabu kubwa ni kuona wanapata ushindi kwenye mechi yao dhidi ya Ndanda FC, itakayopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Juni 20.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mwenyekiti wa Biashara United, Seleman Mataso amesema kuwa kuna hali ngumu inayowakabili Biashara United ila hilo haliwazuii kutafuta matokeo.
“Ni mchezo muhimu kwetu, tunautazama kuwa kipimo ambacho kitaturejesha kwenye ubora tuliokuwa nao wakati ligi inasimama licha ya kwamba hatuna fedha tunahitaji pointi tatu za Ndanda.
“Morali kwa wachezaji ni kubwa na benchi la ufundi limekuwa na ushirikiano mkubwa hivyo ni wakati wetu wa kuonyesha kwamba tupo na tunaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” amesema Mataso.

Biashara United ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 29 kibindoni ina pointi 41.
SOMA NA HII  YANGA YAGOMA KUSHUKA NAFASI YA KWANZA NDANI YA LIGI KUU BARA