Home kimataifa LUKAKU ATABIRIWA KUFUNGA MABAO MENGI KULIKO RONALDO

LUKAKU ATABIRIWA KUFUNGA MABAO MENGI KULIKO RONALDO


NYOTA wa zamani wa Tottenham,Darren Bent anaamini kuwa mshambuliaji wa Chelsea,Romelu Lukaku atafunga mabao mengi zaidi ya Cristiano Ronaldo wa Manchester United. 

Lukaku mwenye miaka 28 amejiunga na Chelsea akitokea Klabu ya Inter Milan kwa mkwanja mrefu ambao ni pauni milioni 97.5 huku Ronaldo akiibuka Manchester United akitokea Juventus. 

Dili la Ronaldo linatajwa kugharimu pauni milioni 15 ambazo mabosi wa United waliweka mezani kumpata staa huyo mwenye miaka 36.

Msimu uliopita Ronaldo aliibuka mfungaji bora ndani ya Serie A ambapo alitupia mabao 29 na Lukaku yeye alikuwa namba moja katika timu yake aliyokuwa ya Inter Milan ambapo alitupia mabao 24.

Nyota huyo amesema:”Nafikiria na kuiangalia Chelsea unaangalia mabao mengi yatapatikana kupitia Lukaku kwa sababu ndiyo mashine ambayo itakuwa mbele. Tunafahamu ubora wa Ronaldo ila kuna Mason Greenwood,  Bruno Fernandes, Rashford na Edinson Cavani angalia sasa asicheze mechi zote tofauti na Lukaku yeye ana uhakika,”


SOMA NA HII  KIPIGO CHA MADRID CHAMTIA KIWEWE TUCHEL....ADAI MCHEZO UMESHAISHA..AITOA CHELSEA...