Home Ligi Kuu KOCHA MTIBWA SUGAR AMLILIA BEKI WAKE WA YANGA

KOCHA MTIBWA SUGAR AMLILIA BEKI WAKE WA YANGA


 KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thiery amesema kuwa kuondoka kwa nyota wake Dickson Job kunampasua kichwa kwa kuwa alikuwa ni mchezaji chaguo namba moja.

Job ambaye kwa sasa ni mali ya Yanga zama zake akiwa Mtibwa Sugar alicheza jumla ya mechi 18 kati ya 19 msimu huu kabla ya kusepa na aliwakosa Mbeya City.

 Thiery amesema kuwa kuondoka kwa wachezaji muhimu kwenye kikosi hicho kunamfanya afikirie kujenga upya kikosi hicho.

“Ujue kuna wachezaji ambao waliondoka na walikuwa ni chaguo la kwanza (Dickson Job) sasa kuondoka kwao inakuwa kazi kujenga ngome upya licha ya kwamba inawezekana.

“Ambacho ninakifanya kwa sasa ni kuendelea kuwajenga hawa ambao nipo nao na nina amini kwamba watafanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo,” amesema.

Mtibwa Sugar kwenye msimamo ipo nafasi ya 14, imecheza mechi 22 na kukusanya pointi 24. Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 9 na ile ya ulinzi imeruhusu mabao 16.

SOMA NA HII  DIDA: BADO TUNA NAFASI YA KUBAKI NDANI YA LIGI