Home Ligi Kuu BARAZA: KAGERA SUGAR ITAREJEA KWENYE UBORA

BARAZA: KAGERA SUGAR ITAREJEA KWENYE UBORA

 


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Kagera Sugar, Francis Baraza amesema kuwa anaamini timu hiyo itarejea kwenye ubora wake ndani ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Kagera Sugar haijawa kwenye mwendo bora kwa msimu huu wa 2020/21 ndani ya ligi kwa kuwa ilianza kwa kusuasua.

Ikiwa ipo nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi 24 imekusanya pointi 25 hali iliyofanya Mecky Maxime ambaye alianza na timu hiyo msimu huu kuwekwa kando na Baraza aliyekuwa Biashara United kwa sasa ameanza kukinoa kikosi hicho.

Baraza amesema kuwa amewaona vijana wake wakiwa na juhudi jambo ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri.

“Vijana wanafanya vizuri na imani yangu ni kwamba tutafanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo na hilo linawezekana kwa sababu nimewaambia wanapaswa wajiamini.

“Ipo wazi kwamba ligi ina ushindani mkubwa hivyo nasi ni lazima tuingie kwenye mechi zetu kwa kufanya jitihada zaidi,” . 

SOMA NA HII  GWAMBINA FC YAKOMAA NA KUBAKI LIGI KUU BARA