Home Ligi Kuu UJUMBE HUU WA YANGA KUTOKA KMC

UJUMBE HUU WA YANGA KUTOKA KMC


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 10.

 Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, KMC ipo nafasi ya tano baada ya kucheza jumla ya mechi 24.

Inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni ni 50 na imecheza jumla ya mechi 23.

Mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba, KMC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 hivyo unatarajiwa kuwa mchezo wenye ushindani ndani ya dakika 90.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari na wanahitaji ushindi.

“Maandalizi yapo vizuri na leo kikosi asubuhi kimefanya mazoezi Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kujiweka sawa na mchezo wetu.

“Utakuwa n mchezo wenye ushindani na imani yetu ni kwamba tutapata matokeo chanya kwani kikosi kipo imara na wachezaji wana morali kubwa,” .

SOMA NA HII  JEMBE: KIPA POLISI TANZANIA LAZIMA AHOJIWE