Home Ligi Kuu JEMBE: KIPA POLISI TANZANIA LAZIMA AHOJIWE

JEMBE: KIPA POLISI TANZANIA LAZIMA AHOJIWE


 BAADA ya kipa wa Polisi Tanzania Mohamed Yusuph, kuokota mabao mawili kwenye nyavu zake, Saleh Ally,’Jembe’ mchambuzi wa masuala ya michezo amesema kuwa kuna haja ya kipa huyo kuhojiwa na uongozi wa timu hiyo.

Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini ilikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi.

Mabao hayo kwenye mchezo wa ligi uliochezwa, Moshi Aprili 18 yalifungwa na mchezaji mmoja ambaye ni Jeremia Kisubi.

Ilikuwa ni dakika ya 16 Kisubi akiwa ndani ya 18 alimtungua kwa kichwa huru Yusuph baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Salum Kimenya.

Bao la pili ilikuwa dakika ya 80 kwa mfungaji yuleyule Kisubi kumtungua tena kipa huyo kwa kichwa akiwa ndani ya 18 akitumia pasi ya Ezekia Mwashilindi ambaye naye alipiga pasi hiyo kupitia mpira uliokufa akiwa nje ya 18.

Ni Idd Moby wa Polisi Tanzania ambaye alipachika bao la kufutia machozi ilikuwa dakika ya 34 naye pia ilikuwa kwa kichwa akiwa ndani ya 18 kwa pasi ya Daruesh Saliboko.

Matokeo hayo yameifanya Polisi Tanzania kubaki na pointi 34 ikiwa nafasi ya 7 huku Prisons ikifikisha jumla ya pointi 34 ipo nafasi ya 9.

Jembe amesema:”Angalia vizuri mabao mawili ya Prisons dhidi ya Polisi Tanzania yamefungwa na Jeremiah Juma Ally. Lakini Polisi wamhoji kidogo kipa wao, uzembe huu ni wa kiwango cha lami au kuna nini?,” .

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA BONGO LEO JUMAPILI