Home Habari za michezo MASTAA SIMBA WAFUNGIWA KUIWINDA VIPERS ….VIGOGO WAPANIA KUMALIZA KAZI MAPEMA….

MASTAA SIMBA WAFUNGIWA KUIWINDA VIPERS ….VIGOGO WAPANIA KUMALIZA KAZI MAPEMA….

Habari za Simba

Wekundu wa Msimbazi Simba SC,  wameingia rasmi kambini kuwawinda Vipers wa Uganda mchezo wa marudiano wa Hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.

Simba wanatarajia kumenyana na Vipers Jumanne ijayo Marchi 7, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema, wachezaji wameingia kambini rasmi  na wanatarajia kuanza mazoezi jioni.

“Huwa tunaanza kambi kabla ya siku tatu au nne kabla ya mchezo lakini kwa kutambua umuhimu wa mchezo huu, tumeanza kambi siku tano kabla ili kuwa tayari zaidi kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe.

“Vipers nao watakuja wakiamini kwamba wanaweza kupata nafasi ya kuvuka japo nafasi yao ni finyu lakini wanaamini wanaweza kutoboa, tumenza kambi mapema ili kukabiliana nao,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  "INONGA WA AFCON SIO HUYU WA SIMBA....ANA UTOTO MWINGI SANA...."