Home Habari za michezo “INONGA WA AFCON SIO HUYU WA SIMBA….ANA UTOTO MWINGI SANA….”

“INONGA WA AFCON SIO HUYU WA SIMBA….ANA UTOTO MWINGI SANA….”

Habari za Simba

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa beki wa timu hiyo, henock Inonga ana utoto mwingi jambo ambalo limekuwa likiighalimu timu yake.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Simba tulikuwa tunavimba beki la AFCON, nilishawahi kuwaambia Inonga akija Simba ana masihara mengi. Inonga wa AFCON sio Inonga wa Simba, ana utoto mwingi.

“Bao la pili tumefungwa sababu yake, Mbangula amemzunguka akajiangusha anajifanya ameumia. Timu inahitaji uiokoe halafu unaleta utoto kama huo? Anatoka anasema ameumia bila kuguswa na mtu yeyote, anaighalimu timu,” amesema Mapovu.

SOMA NA HII  FT: AZAM FC 2-3 YANGA SC.......SOPU AMSOPOA DIARRA MAR TANO...