Home Habari za michezo SHABIKI SIMBA:- KWA MWENDO HUU YANGA BINGWA TENA…MZAMIRU NO 10 TANGU LINI…?

SHABIKI SIMBA:- KWA MWENDO HUU YANGA BINGWA TENA…MZAMIRU NO 10 TANGU LINI…?

Simba SC

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa wapinzani wao, Yanga SC watakuwa mabingwa tena wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu kwa mara ya tatu mfufulizo kutokana na kiwango wanachokionesha.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Yanga kwa jinsi wanavyojituma na uwekezaji walio nao, wana kila sababu ya kuwa mabingwa wa nchi hii kwa mara nyingine tena kwa sababu hawa huu utoto utoto wa kujaribu mechi.

“Benchikha timu yake inacheza hata namba 9 hajulikani, Chama winga, Mzamiru namba 10 tangu lini? Kocha huyu ni mbovu anabebwa tu na CV.

“Kama kocha sio mbovu basi Simba hatuna wachezaji. Una Miquissone yupo nche, unamwekaje Mzamiru namba 10 mtu ambaye ni mkabaji? Simba kwa mwendo tunaoenda nao tusahau ubingwa msimu huu.

“Simba asahau kuhusu ubingwa msimu huu, Yanga ametuacha alama saba ina amaana afungwe mechi mbili na sare moja, ni ngumu sana kwa Yanga hii. Wana ubora na wana wachezaji ambao anayetoka na anayeingia utasema bora aliyetoka,” amesema Mchome.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPANDA LIGI KUU KWA MSIMU UJAO...DTB FC WABADILI JINA ....MCHAKATO MZIMA UKO HIVI...