Home Habari za michezo RASMI…..AUCHO NNJE WIKI TATU YANGA….

RASMI…..AUCHO NNJE WIKI TATU YANGA….

Habari za Yanga leo

IMETHIBITIKA kuwa kiungo wa Yanga, Khalid Aucho atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu, akiuguza jeraha lake baada ya kufanyiwa upasuaji wa mdogo wa goti wa mguu wa kushoto, huku akiruhusiwa kutoka hospitali.

Kiungo huyo amesema hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa muda wa wiki tatu kwa ajili ya kuuguza jeraha lake na baadae ataanza kufuata maelekezo ya madaktari juu ya program ya mazoezi.

Amesema anawashukuru wote waliompa pole na kumuombea apone haraka na kuweza kurejea katika ubora wake na kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya mapambano yaliyopo mbele yao.

“Nashukuru Wananchi kwa dua zao kipindi chote cha upasuaji mdogo wa goti, nimeruhusiwa nitakuwa nje ya uwanja wa muda kwa ajili ya kuuguza jeraha ninaimani kwa kipindi nilichopewa nitakuwa fiti na kurejea uwanjani kuendelea na mapambano,” amesema Kiungo huyo.

Ameongeza kuwa kipindi chote atakachokuwa nje atakuwa na program maalum kwa ajili ya kujiweka foti kabla ya kurejea uwanjani katika mazoezi mepesi na ya ushindani.

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema wataendelea kumkosa kiungo huyo katika michezo miwili iliyosalia ya ligi Kuu kwa sababu ya kuuguza jeraha lake.

“Ni kweli tutamkosa Aucho kwa muda wa wiki tatu nje ya uwanja kwa sababu ya jeraha lake baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti, atakuwa chini ya uangalia kwa kipindi chote atakachokuwa nje na kuanza mazoezi mepesi kwa muda aliopangiwa,” amesema Kamwe.

Aucho ambaye alicheza mechi yake ya mwisho ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly nchini Misri baada ya hapo hakuwepo kwenye kikosi cha Yanga katika michezo miwili za Ligi Tanzania Bara, Namungo FC na Ihefu FC uliochezwa Juzi, uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar-es-Salaam .

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUKABILIWA NA CAF SUPER LEAGUE...SIMBA WARUHUSU MASTAA WAKE KUMWAGILIA MOYO...