Home Habari za michezo PAMOJA NA KUKABILIWA NA CAF SUPER LEAGUE…SIMBA WARUHUSU MASTAA WAKE KUMWAGILIA MOYO…

PAMOJA NA KUKABILIWA NA CAF SUPER LEAGUE…SIMBA WARUHUSU MASTAA WAKE KUMWAGILIA MOYO…

Habari za Simba SC

Klabu ya Simba imetoa mapumziko kwa wachezaji baada ya mechi za ligi kusogezwa mbele.

Simba ilipaswa kucheza na Polisi Tanzania siku ya Jumatano, Mei 24 lakini mchezo huo sasa utapigwa Juni 6 wakati mchezo wa kuhitimisha msimu dhidi ya Coastal Union utapigwa Juni 9.

Taarifa iliyotolewa na Simba imebainisha kuwa wachezaji watarejea mazoezini May 24 kwa ajili ya maandalizi ya mechi hizo ambazo ni za kukamilisha ratiba tu kwa Simba.

Simba imemaliza kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa imejihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao endapo Yanga watashinda taji la kombe la Shirikisho la Azam.

Msimu huu Simba hawakuwa kwenye bahati ya kushinda taji lolote ambapo emepoteza fursa hizo kuanzia Ngao ya Jamii mpaka Ligi Kuu.

Hata hivyo Simba wamebakiwa na Kombe moja ambalo wanaweza kugombea ambalo ni la Caf Super League ambapo mashindano yake yatazamiwa kuanza hivi karibuni.

SOMA NA HII  MENEJA WA KIBU DENIS AWACHANA LIVE SIMBA...KUMBE ISHU NZIMA IKO HIVI