Home Habari za michezo GAMONDI AMPA OKRAH DAKIKA 180 ZA KUMSHAWISHI….,LA SIVYO…..

GAMONDI AMPA OKRAH DAKIKA 180 ZA KUMSHAWISHI….,LA SIVYO…..

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Gamondi, amefichua kuwa winga mpya wa timu hiyo, Augustine Okraha ataonekana uwanjani katika mechi mbili zijazo za Kombe la Mapinduzi ambazo ni sawa na dakika 180.

Okrah amejiunga na Young Africans kwenye usajili wa Dirisha Dogo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bechem United ya Ghana, alitambulishwa juzi Jumapili (Desemba 31) kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, wakati Young Africans ikicheza mechi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri.

Winga huyo ambaye aliwahi kuitumikia Simba SC msimu uliopita, alifanya vizuri aliporejea Ghana kuichezea Bechem United ambapo katika mechi 15 za Ligi Kuu msimu huu, alifunga mabao 9.

Akizungumzia usajili wa Okrah, Gamondi alisema: “Leo (jana) Jumanne pengine anaweza kucheza kwa sababu kifiziki yupo vizuri au mchezo wa mwisho.”

SOMA NA HII  HILI HAPA JIPYA KUHUSU EARBUDS ZA ORAIMO....FREEPOD 4 INAKUJA NA MAUJANJA YOTE YA KISASA...