Home Burudani HILI HAPA JIPYA KUHUSU EARBUDS ZA ORAIMO….FREEPOD 4 INAKUJA NA MAUJANJA YOTE...

HILI HAPA JIPYA KUHUSU EARBUDS ZA ORAIMO….FREEPOD 4 INAKUJA NA MAUJANJA YOTE YA KISASA…

Oraimo

Brand ya oraimo inayodeal na kuuza accessories nchini Tanzania, inatarajia kufanya uzinduzi wa bidhaa yake mpya FREEPOD 4, ambayo ni muendelezo wa earbuds zao za FREEPOD 3 zilizotoka mwishoni mwa mwaka juzi (2021).

Kwa wale watumiaji na wapenzi wa Earbuds, hii bidhaa ni special kwao maana inakuja na muundo mpya wa Sliding Case pamoja na APP rasmi (oraimo sound) utakayotumia kuzi-control buds zako. Pia wameboresha zaidi Betri, Muonekano na Functions zitakazopatikana ndani ya App.

FREEPOD 4 imeboreshwa Zaidi kwenye upande wa betri ambapo, utaweza kusikiliza muziki mwororo   kwa Zaidi ya siku moja na nusu (masaa 35.5). Sio hivyo tu pia inakuja na sifa nyengine ya Active Noise Cancellation.

OraimoSifa hii itakusaidia kusikiliza mziki au kuongea na simu bila muingiliano wa sauti za nje, FREEPOD 4 inazuia sauti za nje (Hautaweza kusikia sauti za watu, vitu vingine pindi ukiweka ON) kwahiyo itakupa uhuru wa kuenjoy kila utakachoko kuwa unasikiliza.

Bidhaa hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 3 March, hivyo itakuwa inapatikana katika maduka yote ya Accessories Tanzania nzima kuanzia siku hiyo.

Hivyo basi wapenda bidhaa za oraimo au wapenzi wa kutumia Earbuds mjiandae kupokea bidhaa hii kali kutoka oraimo.  Kufahamu Zaidi kuhusu bidhaa za oraimo tembelea tovuti yao, https://tz.oraimo.com Au kwenye page zao za mitandao ya ijamii;

 oraimotanzania (@oraimotz) • Instagram photos and videos

SOMA NA HII  IKIWA KESHO SIMBA INAKIPIGA NA RUVU...KAMA KAWA AJIBU ABAKISHWA DAR..PABLO AFUNGUKA HAYA...