Home Habari za michezo KUHUSU ISHU ZA ‘MADEM NA KUJISAHAU’…MZINZE ANYOSHEWA KIDOLE YANGA…AKUMBUSHWA YA NKANE NA...

KUHUSU ISHU ZA ‘MADEM NA KUJISAHAU’…MZINZE ANYOSHEWA KIDOLE YANGA…AKUMBUSHWA YA NKANE NA WENZAKE…

Habari za Yanga

Clement Mzize Jumatano iliyopita alifunga bao lake la tatu katika Ligi Kuu Bara msimu huu wakati Yanga ikishinda 1-0 mbele ya KMC na kujikita zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, lakini kocha aliyemnoa straika huyo chipukizi, Said Maulid ‘SMG’, amemtaka aache kuvimba.

SMG, aliyemnoa Mzize katika timu ya vijana (U-20) ya Yanga kabla ya kupandishwa timu kubwa msimu huu, baada ya kumuona Kwa Mkapa akifunga bao lililoibeba Yanga alisema bado hapaswi kuanza kuvimba na kujiona bonge la straika kwani kuna vitu anahitaji kuvifanya ili awe bora zaidi.

SMG alisema anamjua vizuri Mzize na anaamini anaweza kuwa bora zaidi ya anavyofanya sasa kama ataongeza juhudi na kufanyia kazi kile anachoelekezwa.

“Tangu nikiwa naye timu ya vijana nilikuwa namwambia anahitaji kupambana sana, eneo analocheza hapaswi kuwa mtu wa kuzembea kwani amebeba mabao ya timu, naona analifanyia kazi lakini anahitaji kujiongeza zaidi,” alisema nyota huyo wa zamani wa Yanga, Simba na Taifa Stars na kuongeza;

“Pili anahitaji kuchangamka, kuna muda kocha unaweza kuhisi amechoka kwa namna anavyokimbia kigoigoi au pale timu inapokuwa haina mpira kumbe ndivyo alivyo, anatakiwa kubadilika haraka na kuendana na kasi ya timu.”

Pia winga teleza huyo wa zamani, alimtaka straika huyo asivimbe kichwa na kujiona supastaa, ila ajifunze kwa wakali alionao kikosini.

“Uzuri ameingia Yanga ikiwa na washambuliaji bora kama Mayele (Fiston), hivyo anahitaji kujifunza kwake maana ana kila kitu bora, asijione amefika, wakati bado ana safari ndefu na kama atakuwa na nidhamu, na kuendelea kujifunza basi anaweza kutisha zaidi hapo baadae,” alisema SMG.

Nafasi anayocheza Mzize pia ina wakali wengine kama Kennedy Musonda, Crispin Ngushi na viungo washambuliaji Stephane Aziz KI, Bernard Morrison, Farid Mussa, Dickson Ambundo, Denis Nkane, Tuisila Kisinda na Jesus Moloko.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AANZA NA KUTATUA TATIZO LA UBUTU WA SARPONG