Home Habari za michezo BAADA YA KUMBONDA VIPERS KWAKE….SIMBA WAANZA NGEBE UPYA…WATOA MSIMAMO WAO KWA CAF…

BAADA YA KUMBONDA VIPERS KWAKE….SIMBA WAANZA NGEBE UPYA…WATOA MSIMAMO WAO KWA CAF…

Habari za Simba

Uongozi wa Simba, umetoa tamko kwamba, wapinzani wao wa kimataifa ambao wana zamu ya kushuka Uwanja wa Mkapa jijini Dar, watakutana na pumzi ya moto ambayo itakuwa simulizi kwa wengine.

Mchezo wa kwanza Simba kutupa kete yake Uwanja wa Mkapa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi msimu huu, ilikutana na kitu kizito baada ya kuchapwa mabao 0-3 dhidi ya Raja Casablanca.

Akizungumza nasi, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, alisema: “Raja Casablanca walikuwa bora kwa siku hiyo, wakapata ushindi, lakini Horoya na Vipers lazima watakutana na pumzi ya moto ili wakawasimulie wengine.

“Haina maana kufungwa na Raja Casablanca watakaokuja wataendelea kupata ushindi, hilo wasahau, lazima tuwaambie kwamba hii ni Dar na pale ni Benjamini Mkapa, hivyo lazima tuwapalekee pumzi ya moto.

“Mashabiki waliumia na maumivu haya yapo kwetu, lakini huo mchezo umeshapita na sisi tumechagua kusonga mbele kwa kuwa lazima mapambano yaendelee na tupo tayari, wageni wakaribie, watapata kile kinachowastahili kabisa.

Juzi Jumamosi Simba walipata ushindi wa goli 1-0 mbele ya Vipers na kufufu matumaini ya kufuzu hatua ya Robo fainal kutoka kwenye kundi lao ambapo wanaaama 3 wakitanguliw ana Raja Casablanca mwenye alama 9 na Horoya wenye alama 4.

Mechi Ijayo Simba wataikaribisha Vipers Jijini Dar es Salaam, ambapo wanatazamia kuibuka na ushindi kwa hali na namna yoyote ile huku wakiomba Raja wamfunge Horoya ili wapande mpaka nafasi ya pili.

SOMA NA HII  DOUMBIA KUMBE HAJAMALIZANA NA YANGA, ISHU IKO HIVI