Home Uncategorized GWAMBINA FC YAWASHUSHA PRESHA MASHABIKI,DAKIKA 360 YAFUNGWA MABAO MATANO

GWAMBINA FC YAWASHUSHA PRESHA MASHABIKI,DAKIKA 360 YAFUNGWA MABAO MATANO

 


NOVATUS Fulgence, Kocha Mkuu wa Klabu ya Gwambina FC ya Mwanza amesema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara licha ya kushindwa kuambulia pointi kwenye mechi zake za ligi.


Gwambina FC ikiwa imeyeyusha dakika 360 kwenye mechi zake nne za ligi kuu imeshindwa kuambulia ushindi wala bao la kufunga.


Ilianza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Biashara United, ikalazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting na mchezo wake wa nne ilichapwa mabao 3-0 mbele ya Simba.

Jumla imeruhusu mabao matano kwenye mechi zake nne huku safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Paul Nonga ikiwa haijafumania nyavu.

Kocha huyo amesema:”Bado tupo imara kwa kuwa makosa madogo ambayo tumekuwa tukiyafanya yanarekebishika na ndiyo ambayo tunayafanyia kazi kwa sasa.


“Kikubwa mashabiki wasikate tamaa bado tupo imara na tuna nafasi ya kuweza kupata matokeo kwenye  mechi zetu zijazo huu ni mwanzo wa ligi bado tuna mechi nyingi za kucheza na tutashinda.”

SOMA NA HII  MWANUKE BYE BYE SIMBA