Home Uncategorized SIMBA YAIPIGIA HESABU TANZANIA PRISONS

SIMBA YAIPIGIA HESABU TANZANIA PRISONS


MABINGWA watetezi wa Simba wameanza kuivutia kasi Klabu ya Tanzania Prisons kwa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa Juni,28 Uwanja wa Sokoine.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 yaliyojazwa kimiana na John Bocco kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City.

Wapinzani wao Tanzania Prisons wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Tanzania kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

Tanzania Prisons ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Adolf Rishard hesabu zake kubwa ni kumaliza ligi ikiwa ndani ya 10 bora msimu huu wa 2019/20.

Simba inahitaji pointi tatu ili kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo wanahitaji kuutwaa ubingwa wakiwa na mechi nyingine mkononi.

Timu zote zimecheza mechi 31 ambapo zimebakiwa na mechi saba mkononi kwa sasa.

 Mchezo wao uliopita Uwanja wa Uhuru, Simba ilitoshana nguvu ya bila kufungana na Tanzania Prisons hivyo kazi itakuwa kubwa pale watakapokutana ndani ya uwanja.

Rishard amesema:”Tunahitaji kufanya vizuri mchezo wetu ujao, tutakutana na timu nzuri na ngumu ila tupo tayari.”

Sven amesema:”Ni mchezo muhimu na mgumu kwetu hilo tunalitambua hivyo wachezaji wana kazi ya kusaka pointi tatu kutimiza malengo.”

SOMA NA HII  HIZI HAPA MECHI ZA YANGA NDANI YA LIGI KWA MWEZI SEPTEMBA