Home Uncategorized SWALA LA MKWABI NDANI YA SIMBA LAIBUKA UPYA…TFF WATOA TAMKO HILI..!!

SWALA LA MKWABI NDANI YA SIMBA LAIBUKA UPYA…TFF WATOA TAMKO HILI..!!

KLABU ya Simba na vyama kadhaa kikiwamo kile cha Makocha (TAFCA) na Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) vimeshikwa pabaya baada ya kutakiwa kuitisha haraka chaguzi ndogo za kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwa muda mrefu sasa kinyume cha katiba zao.

Mbali ya TAFCA na DRFA, chama kingine kinachotakiwa kufanya uchaguzi wao ni kile cha Mkoa wa Songwe ambao tayari wameshaanza mchakato wao kwa sasa.

TAFCA wanatakiwa kufanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wao Wilfred Kidao ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anayoishikilia tangu mwaka jana.

Upande wa DRFA, nao wanatakiwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Almasi Kasongo ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPBL) nafasi aliyoipata mwaka huu.

Tayari vyama hivyo na vingine sambamba na klabu zimeshapewa maelekezo na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, ambapo Mwenyekiti wake, Ally Mchungahela amesema kwa klabu zinatakiwa kufanya chaguzi zao mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Bara.

Mchungahela aliiambia Mwanaspoti; “Vyama vya mikoa na vingine ambavyo vinatakiwa kufanya uchaguzi wao mkuu ama mdogo kuziba nafasi tumewaelekeza wafanye hivyo kuanzia hivi sasa kwani muda umepita.

“Ukiangalia kuna vyama ambavyo viongozi wao wameondoka muda mrefu lakini hawajaziba nafasi, hivyo tumewapa taarifa juu ya hilo na wanatakiwa kutekeleza kwa mujibu wa Katiba.

“Kwa upande wa klabu wakiwemo Simba wanapaswa kufanya uchaguzi wao mara baada ya ligi kumalizika.

“Katiba zao zipo wazi kwamba kiongozi akiondoka kwa sababu yoyote ile basi uchaguzi unapaswa kufanyika baada ya miezi mitatu lakini vyama na klabu hazifanyi hivyo.

“Ni jukumu la kila mmoja kufuata Katiba inavyoongoza sio lazima kukumbushana, huku ni kuvunja Katiba za vyama na klabu,” alisema Mchungahela.

Simba inatakiwa kuziba nafasi ya Swedy Nkwabi aliyejiuzulu Uenyekiti Septemba mwaka jana na nafasi yake kukaimiwa na Mwina Kaduguda, huku ikielezwa uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo utafanyika baada ya Uchaguzi Mkuu wa Taifa unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

SOMA NA HII  KAZE ATUA BONGO, KUANZA MAJUKUMU YANGA