Home news PAMOJA NA SAKHO KUANZA KUKIWASHA MSIMBAZI…MECHI YA KESHO ATAISHIA KUITAZAMIA JUKWANI

PAMOJA NA SAKHO KUANZA KUKIWASHA MSIMBAZI…MECHI YA KESHO ATAISHIA KUITAZAMIA JUKWANI


Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, amerejea mazoezini pamoja na wachezaji wenzake baada ya kupona jeraha la mguu lililokuwa linamsumbua.

Sakho alipatwa majeraha katika mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Uwanja wa Jamhuri mwanzoni mwa mwezi huu.

Pamoja na kuanza mazoezi Sakho bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari ili kuhakikisha anapona jeraha lake na kuwa sawa tayari kwa kuanza kucheza tena kwenye mechi mbalimbali za Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, uwezekano wa Sakho kuwepo katika kikosi kitakachocheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy Jumapili ni mdogo kutokana na kutokuwa fiti asilimia 100.

SOMA NA HII  SIMBA INAKWAMA HAPA...PABLO, MUGALU WAIBUKA NA YAO...EDO KUMWEMBE AMTAJA CHAMA...