Home BIashara United WAKATI MECHI YAO DHIDI YA WALIBYA NI LEO..BIASHARA UNITED BADO WAPO TZ…TFF...

WAKATI MECHI YAO DHIDI YA WALIBYA NI LEO..BIASHARA UNITED BADO WAPO TZ…TFF YATUMA BARUA CAF..

TFF imeliomba Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kusogeza mbele mchezo wa kati ya Al Ahly Tripoli ya Libya dhidi ya Biashara United ya Tanzania hadi Oktoba 27, 2021. TFF imesema licha ya kupatikana ndege ya kukodi safari imeshindikana kwa sababu ya kukosekana vibali vya anga.

Biashara United ya Tanzania hadi sasa haijasafiri kwenda Libya kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli, kutokana na changamoto za usafiri wa anga. Mchezo huo umepangwa kuchezwa leo saa 2:00 usiku. Katika mchezo wa kwanza Biashara ilishinda 2-0.

Mpaka sasa bado haijatolewa taarifa rasmi iwapo CAF wameridhia maombi hayo ya kusogeza mbele mchezo huo.




SOMA NA HII  GAMONDI ATAMBA SIO MTU MMOJA MMOJA NI KIKOSI KIZIMA ETI......ISHU IKO HIVI