Home Simba SC MASAU BWIRE AKERWA NA “BUSHA” LA MORRISON

MASAU BWIRE AKERWA NA “BUSHA” LA MORRISON

ILE staili ya ushangiliaji ya nyota wa Simba, Benard Morrison kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Al Hilal ya Sudan imezua mijadala huko mitandaoni na mmoja wa wadau ambaye hajapitwa na hilo ni Masau Bwire.

Kama ambavyo mnamfahamu Masau Bwire ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Instagram kusema kile aombacho mtu hupewa. Hakuishia hapo, maneno yake yalisomeka, “Aombacho mtu hupewa. Huyu bingwa naona anaomba kutune kama mpira wa miguu. Kwa kuwa Mungu si Athumani, siku ombi lake likijibiwa, asipige kelele.”

Masau akatoa nafasi kwa wafuasi wake kwa kuwauliza wanasemaje juu ya tukio lile, wapo ambao walikuwa wakimuunga mkono kutona na alichokiandika lakini asilimia kubwa ya mashabiki wa Simba waliona ni kama msemaji huyo wa Ruvu Shooting anawaonea wivu tu.

Hivi karibuni kulikuwa na maneno kuwa Mghana huyo alikuwa akiumwa kitu ambacho alikanusha kwamba hakuwa mgonjwa wa kile ambacho walikuwa wakikisema ndio maana alishangilia vile.

SOMA NA HII  MISHAHARA YA WACHEZAJI YANGA KULIPWA MASTAA SIMBA WAKISHINDA KESHO...MO DEWJI AFANYA KUFRU...