Home Ligi Kuu ZIKIWA ZIMESALIA SIKU NNE KABLA YA SIMBA vs YANGA….RATIBA LIGI KUU YAPANGULIWA...

ZIKIWA ZIMESALIA SIKU NNE KABLA YA SIMBA vs YANGA….RATIBA LIGI KUU YAPANGULIWA KIMYA KIMYA…


WAMEKOSEKANA ndivyo unavyoweza kusema baada ya wachezaji wa Simba, Yanga kukosekana kwenye timu ya Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki.

Hii inatokana na wachezaji wa timu hizo kukosekana kwenye kikosi cha nyota 23, kilichoitwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa Kimataifa wa kusheherekea miaka 60 ya Uhuru dhidi ya Uganda.

Licha ya kutotolewa ufafanuzi juu ya kukosekana kwao ila  sababu ni mchezo unaofuata baina ya timu hizo unaotarajiwa kuchezwa Desemba 11.

Mechi hiyo ya kirafiki inapangua ratiba ya michezo iliyopangwa kuchezwa siku hiyo ambayo ingewakutanisha Mtibwa Sugar na Biashara United, na mchezo mwingine ukihusisha Azam FC dhidi ya Kagera Sugar kutokana na wachezaji wa timu hizo kujumuishwa kwenye kikosi cha Stars.

Nyota waliojumuishwa katika kikosi cha Stars ambao mechi zao zilipaswa kuchezwa Desemba tisa ni Lusajo Mwaikenda, Sospeter Bajana (Azam FC), Abdulmajid Mangalo, Denis Nkane (Biashara United) na Meshack Abraham wa Kagera Sugar.

Kikosi kilichoitwa kwenye mchezo huo ni Metacha Mnata (Polisi Tanzania), Haroun Mandanda (Mbeya City), Musa Mbisa (Coastal Union), Nathaniel Chilambo (Ruvu Shooting), Kelvin Kijiri (KMC), Hans Masoud (Coastal Union) na Nickson Kibabage (KMC).

Oscar Masai (Geita Gold), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Nashon Naftal (Geita Gold), Tariq Simba (Polisi Tanzania), Sospeter Bajana (Azam FC), Hassan Nassor (Dodoma Jiji), Abdul Suleiman ‘Sopu’ (Coastal Union).

Wengine ni Meshack Abraham (Kagera Sugar), Cleophace Mkandala (Dodoma Jiji), Denis Nkane (Biashara United), Rashid Juma (Ruvu Shooting), Vitalis Mayanga (Polisi Tanzania), Anuary Jabir (Dodoma Jiji) na Reliant Lusajo wa Namungo FC.

Nyota hao wanatarajiwa kuingia kambini leo Desemba 6, kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo.

SOMA NA HII  MABINGWA WOTE WA MASHINDANO YA CAF NI KUJICHOTEA MABILIONI YA PESA...SIMBA WAKIKAZA TU WAMO...