Home Habari za michezo LIGI YA MABINGWA AFRIKA…SIMBA NDIO KWANZAA KUNAKUCHA…HOROYA AKIONA CHA MTEMA KUNI…

LIGI YA MABINGWA AFRIKA…SIMBA NDIO KWANZAA KUNAKUCHA…HOROYA AKIONA CHA MTEMA KUNI…

Simba vs Vipers

BAO la Clatous Chama alilofunga dakika ya 45 limetosha kuipa Simba ushindi katika mchezo wao dhidi ya Vipers uliochezwa jana katika uwanja wa Mkapa.

Chama alifunga bao hilo akitumia vizuri pasi ya Moses Phiri ambaye alimpenyezea na yeye kuweka wavuni.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi sita na mabao mawili ikishika nafasi ya pili katika kundi C huku nafasi ya kwanza ikiwa ni Raja Casablanca ikiwa na pointi 12 baada ya kuichapa Horoya mabao 3-1 jana.

Simba imeendeleza ubabe kwa Vipers kwenye mechi mbili mfululizo ikishinda nyumbani na ugenini katika hatua hii ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo wa kwanza nchini Uganda, Simba ilishinda 1-0 bao likifungwa na Henoc Inonga na kwenye mchezo wa Mkapa imeshinda tena 1-0.

Nafasi ya tatu ipo Horoya ikiwa na pointi nne huku Vipers ikishika mkia ikiwa na pointi moja pekee.

Simba itakuwa barua kingine cha kusaka pointi tatu mbele ya Horoya Machi 18 katika uwanja wa Mkapa huku Vipers ikiisubiri Raja Casablanca nchini Uganda.

SOMA NA HII  RASMI....FIFA WAMTAJIRISHA MSUVA CHAP CHAP....WAARABU WAAMRIWA WAMLIPE BILIONI 1.6...ISHU NZIMA IKO HIVI....