Home Habari za michezo KOCHA WA CHELSEA AFUNGA SAFARI MPAKA BONGO KUMTAZAMA MUSONDA LEO…ALIANZA NA CHAMA...

KOCHA WA CHELSEA AFUNGA SAFARI MPAKA BONGO KUMTAZAMA MUSONDA LEO…ALIANZA NA CHAMA JANA..

Habari za Yanga

KAMA utakuwa uwanjani leo wakati Yanga ikiikaribisha Real Bamako ya Mali katika mechi ya Kundi D ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, basi ujue mapema jukwaa la VVIP kutakuwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Avram Grant.

Kocha huyo raia wa Israel atakuwa Kwa Mkapa kwa ajili ya kumcheki straika wa Yanga, Kennedy Musonda, aliyemteua miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo anayoifundisha kwa sasa.

Tayari Chama cha Soka Zambia (FAZ), kimeitumia barua Yanga kikiitaarifu juu ya ugeni huo ambao utakuwa maalum kwa Yanga, pia kwa Musonda ambaye ndio lengo kuu.

Katika barua ambayo Yanga imetumiwa na FAZ pia kimeiomba Yanga kuandaa kikao maalum kwa Grant na Musonda kukutana katika kikao kifupi.

Huenda kocha huyo pia alikuwa uwanjani jana kumtazama kiungo wa Zambia, Clatous Chama wa Simba ambaye aliifungia timu yake goli muhimu  kwenye mechi ya Kundi C ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers ya Uganda.

Grant anataka kuja kumsoma Musonda kabla hajafanya uamuzi wa mwisho wa kumjumuisha kwenye kikosi cha Chipolopolo kitakachocheza mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (AFCON).

Tayari Musonda ameshaanza kuuwasha moto kwenye mechi za makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo katika mabao manne ambayo Yanga imefunga amefanikiwa kufunga bao moja.

Mbali na kukutana na Musonda pia Grant atakuwa na kikao kifupi na kocha wa mshambuliaji huyo Nasreddine Nabi kabla ya kesho yake kuondoka nchini.

Katika mchezo huo ambao Yanga inahitaji ushindi kuongeza hesabu zao za kutinga hatua ya robo fainali Mwanaspoti linajua kuwa Musonda ana nafasi kubwa ya kuanza baada ya mazoezi yao ya jana.

MSIKIE KAMWE

Ujio wa Grants umethibitishwa na Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe akisema kocha huyo ambaye pia amewahi kuifundisha West Ham United ya England na timu ya taifa ya Ghana.

“Tunaposema Kwa Mkapa ni Full Shangwe hii ni moja ya tukio kubwa siku ya mchezo wetu dhidi ya Real Bamako, hebu fikiria kocha mkubwa kama huyu anakuja kwa Mkapa akitoka mbali huko alafu mtu awe yuko Tegeta au Temeke abaki nyumbani, nalithibitishia kwamba ni kweli klabu itampokea huyu kocha mkubwa kwa ziara maalum hapa kwetu,”alisema Kamwe.

SOMA NA HII  KUMEKUCHA FEI TOTO ATAKA KULIANZISHA TENA AZAM, ADAI HANA FURAHA