Home Uncategorized SIMBA:TUNAITAKA NGAO YA JAMII, TUTAPAMBANA MBELE YA AZAM FC

SIMBA:TUNAITAKA NGAO YA JAMII, TUTAPAMBANA MBELE YA AZAM FC


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna namna yoyote ile watakayofanya mbele ya Azam FC kwenye mchezo wao wa ngao ya jamii zaidi ya kushinda na kutwaa ngao hiyo.

Simba itashuka uwanja wa Taifa, Agosti 17 kumenyana na Azam FC kwenye mchezo huo maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 23.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hakuna kingine ambacho wanakiwaza kwa sasa zaidi ya kutwaa ngao ya jamii.

“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu kwetu nasi tunajipanga kufanya vema mbele ya wapinzani wetu Azam Fc, ni timu bora na makini ila hakuna namna tunahitaji ushindi na kutwaa ngao ya jamii,” amesema.

SOMA NA HII  BEKI SIMBA AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA