Home Uncategorized BEKI SIMBA AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

BEKI SIMBA AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA


GADIEL Michael, beki wa Simba anayevaa jezi namba mbili amesema kuwa wakati huu ni muhimu kila mmoja akachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Beki huyo amesema kuwa kitu cha muhimu kwa kila mmoja ni afya hivyo ni muhimu kufuata kanuni na taratibu za Wizara ya afya ili kuwa salama.

“Ni janga kubwa ambalo lipo kwa taifa na dunia nzima kiujumla ila ni muhimu kufuata utaratibu ambao umewekwa na Serikali kwa kuchukua tahadhari.

“Mimi pia ninachukua tahadhari hivyo nina amini hata wewe pia unaweza kuchuka tahadhari ili uwe salama,” amesema Gadiel.

SOMA NA HII  MITAMBO INAYOMPA JEURI MGUNDA