Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUTUPWA NNJE LIGI YA MABINGWA…MANARA ASHINDWA KUJIZUIA…ABADILI GIA ANGANI...

BAADA YA YANGA KUTUPWA NNJE LIGI YA MABINGWA…MANARA ASHINDWA KUJIZUIA…ABADILI GIA ANGANI ‘CHAP’ HARAKA…

Habari za Yanga

Ofisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amewatuliza wachezaji wa Yanga baada ya kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kipigo cha bao 1-0 na AL Hilal juzi Jumapili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika; “Football haipo vile tunavyodhani Sisi huku mtaani, wala sio mchezo wenye guarantee ya matokeo utakayo wewe.

Watu wa kisasa wanasema ni mchezo katili, ila tuongezee na bahati, tusipoipata hii na kukubali pia kuna Mipango ya Mungu, tutakuwa hatuitendei haki football yetu.

Rudini mjipange na linalokuja Wachezaji wetu, msihisi Dunia imewaangukia nyie, mna nafasi ya kurejesha heshma yenu wiki ijayo na kurejesha furaha yetu, Uwezo huo mnao, ni fursa adhimu ya kuthibitisha mliteleza na hamkuanguka.

Nawasihi sana sahauni ya Sudan, rejesheni ari na nguvu Jumapili ijayo kisha msubirie kombe la Shirikisho. Bado tuna Imani na nyie na tunajua mtatufurahisha next weekend Insha’Allah.”

SOMA NA HII  YANGA JIANDAENI..PABLO AANZA NA MAMBO MATATU SIMBA..MORRISON NDANI...CHAMPION LEO..